WELCOME TO BOAZ FOUNDATION TANZANIA

OVECOMERS POWER CENTER, ENDTIME HARVEST CHURCH,OVERCOMERS FM RADIO IRINGA,OVERCOMERS MINISTRY TO THE NEEDY.

Friday, May 11, 2012

ASKOFU BOAZ SOLLO ATUMIA JINA LA YESU KUKOMESHA MAPEPO, IMANI ZA KISHIRIKINA KATIKA SHULE YA MSINGI ILALA
Wanafunzi waliokusanyika kwaajili ya maombi

Askofu wa makanisa ya OPC na EHC Tanzania Boaz Sollo leo amefika katika shule ya msingi ilala iliyopo katika manispaa ya Iringa Baada ya wanafunzi kusumbuliwa kwa muda wa zaidi ya wiki mbili.
Askofu Sollo alifika shuleni hapo asubuhi baada ya kupokea mualiko kutoka kwa  uongozi wa shule hiyo ili afanye maombi shuleni hapo pamoja na kwa wanafunzi. Ambapo alipofika  akafanya maombi katika shule hiyo na hali kutulia na wanafunzi kuendelea na masomo yao kama kawaida.

kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule hiyo  John Nyoni anaeleza kuwa WANAFUNZI wa kike zaidi ya 14 katika shule hiyo hadi alipofika askofu walikuwa tayari wamekubwa na ugonjwa wa ajabu wa kuanguka na kuweweseka (kusema maneno yasiyojulikana) kwa zaidi ya wiki moja sasa .
Nyoni anaeleza kuwa tatizo hilo la wanafunzi kuanguka na kuweweseka lilianza kuwakumba wanafunzi hao zaidi ya wiki mmoja sasa.
Nyoni alisema kuwa awali alianza kuanguka mwanafunzi mmoja ila kila wakati kwa kipindi cha wiki mbili sasa wanafunzi wamekuwa wakianguka na kufikisha idadi ya wanafunzi 14 hadi leo.

Alisema kuwa wanafunzi ambao wamekuwa wakikumbwa na tatizo hilo ni wale wa kike ambao ni darasa la saba na kuwa mara baada ya kuanguka pindi wanapoamka wamekuwa wakikimbia na kusema maneno ambayo ni vigumu kwa mtu mwingine kujua maana na maneno hayo.

Aliwataja wanafunzi ambao wameanguka kuanzia juzi hadi leo kuwa ni Afsa Mkelemi, Husna Lwila, Subira Hamisi, Regina Mlowe, Anna Hongoli, Ramla Yassin , na Neema Raphael na kuwa wanafunzi hao ndio walioanguka kuonekana kuzidiwa zaidi .

Hata hivyo mkuu huyo wa shule alisema kuwa tayari uongozi wa shule hiyo umechukua hatua mbali mbali za kutatua tatizo hilo ikiwemo ya kuwaita viongozi mbali mbali wa madhehebu ya dini zote .

Baada ya kufanya maombi Askofu Sollo amewataka wanafunzi na waalimu kuondokana na dhana ya woga na kumtegemea Mungu kupitia Yesu Kristo maana yeye ndiye mwenye kuweza kutatua matatizo yote.


Thursday, April 26, 2012

Umati wa wakazi wa Iringa waliofika mbele kwaajili ya kuokoka na kuombewa na Askofu Dr Boaz Sollo
Mmoja wa waliopokea muujiza baada ya kuombewa akitoa ushuhuda mbele ya kanisa kulia Askofu Sollo akimsikiliza.
Askofu Boaz sollo akiongea na waumini OPC na wenye shida mbalimbali waliofika katika siku hii maalumu kwa maombi ya mtu mmoja mmoja.


Askofu Dr Boaz Sollo akifungua kwa maombi kabla hajaanza kuombea mwenye uhitaji mmoja mmoja aliyehudhuria katika ibada hiyo ya maombezi wengi walifunguliwa.
Congregation at IDYDC Hall
ONE TO ONE PRAYER MIRACLE AT IDYDC HALL IRINGA

With Bishop Boaz Sollo of Endtime and OVERCOMERS POWER CENTER.
Many get healed and released from satan strongholds.


Askofu Dr Boaz Sollo wa makanisha ya Endtime Harvest church (EHC) na kituo cha maombezi Overcomers Power Center (OPC) wiki hii amendaa huduma ya maombezi kwa mtu mmoja mmoja ambayo itafanyika katika ukumbi wa IDYDC mkoa wa Iringa.
Ibada hizo ambazo hufanyika kila siku ya Alhamisi na Jumapili kuanzia saa nane hadi 12 jioni zimekuwa zenye mafanikio kutokana na watu kufunguliwa katika vifungo vya shetani na kuponywa magonjwa yalio gumzo kutokana na kutokuwepo na matibabu kama Ukimwi na mengineyo.
Katika siku ya alhamisi ya leo katika maombi ya mtu mmoja mmoja baada ya maombi hayo kijana Ansidal Ngoi (17) kutoka Welu mkoani Iringa anashuhudia kuponywa kabisa kifafa ambacho kilianza msumbua toka alipokuwa na miaka mitatu. Ngoi aliendelea kuweleza kuwa alijikuta akishambuliwa na kifafa hicho mara tatu au tano kwa siku nakueleza kuwa ni mwezi mmoja umepita na hali hiyo haijarudia tena. Amewataka wote wenye matatizo na shida mbalimbali kutosita kufika katika huduma ya OPC kwa maombezi kwani ni kweli kwamba Askofu Sollo anaye Mungu wa kweli.
Naye kijana Philipo Stephano toka Misele anashuhudia kuwa mwaka 2007 alipima afya akagundulika kuwa ana Ukimwi lakini baada ya kuombewa na Mtumishi wa Mungu ndipo alipochukua hatua ya kupima tena majibu yalionesha kuwa hana ukimwi.
Mama aliyekuwa mjamzito na sasa anamtotowa kiume kwa jina Joshua anatoa ushuhuda kuwa alianza kuhudhuria katika huduma hiyo toka miezi mitatu iliyopita. Katika ujauzito aliokuwa nao ulimletea matatizo ya kila mara lakini kutokana na huduma ya maombi alipata uponyaji. Wakati wa kujifungua ulifika lakini siku ziliendelea kupita ndipo tena alipoombewa akapata dalili ya uchungu na alipofika hospitali akajifungua salama.
 Naye Askofu Boaz Sollo aliwaasa kwa wale wanaofika katika ibada hizo kwaajili ya kuombewa na kuondoka kutofanya hivyo kwani. Baada ya kuponywa wanatakiwa wapate masomo ambayo yatawaimarisha katika Imani na kuwa na nguvu za kukabiliana na shetani. 

Katika maombi hayo yaligawanywa kwa makundi mbalimbali wakiwemo watoto wadogo kuanzia miaka 13 ambao wanapigwa vita sana na shetani na mara nyingi watoto wamejikuta na watoto kutokana na kukosa nguvu ya Roho wa Mungu na kukosa maadili au malezi bora, Pia kabla ya kuwaombea aliwataka wototo wote wenye simu na walio katika mahusiano ya kimapenzi kufuta namba za wapenzi hao na kuzingatia malengo yao ya kimaisha. 
Kundi lingine ni Wenye vizuri vya ukimwi, wasio na watoto, wenye vifafa na  degedege pamoja na wamama wajawazito.

Thursday, April 12, 2012




Watoto waliohudhuria katika kipindi cha watoto kinachorushwa na Radio ya Overcomers 98.6 fm wakiwa na Aunt Adella kivaly ambaye ndie muongozaji wa kipindi hicho.Baada ya kukabidhiwa zawadi toka OCC.
Bishop Dr Boaz Sollo on a group picture with the Guest of Honor during the distribution of Gifts from Operation Chrismas Child (OCC), More than 25,000 Children from Iringa are expected to receive those gift.
Mratibu wa OCC na Mwangalizi wa makanisa ya OPC na EHC Tanzania akikabidhi zawadi kwa watoto

Watoto wakizifurahia zawadi hizo baada ya kuzipokea
Hapa wakizifungua zawadi hizo kutambua kilichopo ndani
Watoto wakiwa wamenyanyua zawadi baada ya kukabidhiwa
Baadhi Mabox ya Zawadi kutoka OCC
OPERATION CHRISTMAS CHILD OCC YATOA ZAWADI IRINGA
Shirika la kimataifa linalohudumia watoto walio katika mazingira walio katika mazingira magumu jana kupitia muwakilishi wa shirika hilo hapa Nchini kwa mkoa wa Iringa Dr Boaz Sollo aliongoza zoezi la ugawaji wa zawadi kwa watoto.

Zoezi hilo la ugawaji wa zawadi lilifanyika katika ukumbi wa IDYDC Mkoani wa Iringa ambapo watoto walikusanyika pamoja na viongozi mbalimbali wa kanisa kama wawakilishi na kukabidhiwa zawadi hizo.

Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi kwa niaba ya mwenyekiti wa OCC kitaifa Askofu Rodrick Mbwambo, Dr Bishop Boaz Sollo ambaye ni msimamizi wa makanisa ya ENDTIME HARVEST CHURCH na OVERCOMERS POWER CENTER(OPC), alieleza kuwa historia ya ugawaji zawadi hapa nchini umeanza kwa kipindi cha miaka kumi kwa sasa.

Dr Sollo ameongeza kuwa OCC inapeleka zawadi katika nchi 130 duniani kote ikiwemo Tanzania, huku kwa mkoa wa iringa ukiwa ni mwaka wa tatu toka zawadi hizi zianze kugawiwa kwa watoto wasiojiweza na wanaoishi katika mazingira magumu. Aliongeza kuwa zawadi hizo zinatolewa kupitia makanisa yote Iringa yaliyotayari kushirikiana na kamati ya OCC mkoani Iringa.

Mwaka huu koa wa iringa umeongezewa idadi ya mabox ya zawadi kutoka 3500 mwaka jana hadi 6,500 ambapo box moja lina thamani ya Tsh 30,000 na kufanya zawadi hizo kwa mkoa wa iringa kuwa na thamani 111,000,000.


Mbali na iringa OCC imefanikiwa kupeleka zawadi hizi mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro,Mbeya, Lindi, Pwani na Dar es Salaam. Huku kukiwa na matarijio ya kupata zawadi mara mbili zaidi ili kuwezesha kufikia wilaya zote za mkoa wa Iringa na mingineyo.

Dr Sollo aliishukuru Serikali kwa kusamehe kodi ya ushuru kwa makontena ya zawadi na kuomba serikali ya Tanzania kutumia mamlaka ya bandari kuweka mfumo rahisi wa kutoa zawadi wa kutoa vitu bandarini kwani kila kila mwaka wanalazimika kulipa mamilioni ya fedha yajulikanayo kama "storage charge".

Pia Dr Sollo alitoa tahadhari kwa serikali kuwa makini kwa yeyote atakayejaribu kuhatarisha amani kwa kutumia dini au siasa.

Naye muwakilishi wa Mgeni rasmi Joseph Nyikani afisa elimu mkoa wa iringa alitoa shukrani kwa uongozi wa OCC kwa kuutambua umuhimu na kumualika Mkuu wa mkoa Dr. Christine Ishengoma kuwa mgeni rasmi. Aliweka msisitizo kwa watoto ambao wengi ni wanafunzi kuzingatia Elimu kwani elimu ndio msaada mkuu katika maisha yao ya sasa na baadae.

Aliongeza kuwa kwa kuwa mbali na OCC kutoa zawadi inatoa elimu ya maadili ambapo maadili mengi yameonekana kushuka kutokana na elimu hiyo kupuuziwa na kutoa wito kwa wazazi kuwafunza watoto wao ili taifa liwe lenye maadili maana mmomonyoko wa maadili unapoteza sifa ya taifa.





Monday, March 19, 2012

THE CERTIFICATE AWARDED TO BISHOP DR,BOAZ SOLLO FROM JAPAN BIBLE INSTITUTE
Wafanyakazi wa kituo kinachomilikiwa na Dr. Boaz Sollo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutunukiwa shahada ya udaktari.
Bishop Dr. Boaz Sollo on group photo during his graduation ceremonies
BISHOP DR.BOAZ SOLLO ON A GROUP PHOTO WITH HIS SERVANTS OF OPC




DR.BOAZ SOLLO speak to the invited guests during his graduation ceremony





Taasisi ya Biblia ya Japan imemntunuku Askofu Boaz Sollo Shahada ya udaktari wa falsafa ya Theolojia Doctorate degree in Divinity.

Askofu Sollo amehitimu masomo ya Theolojia katika Taasisi hiyo, kwa sasa jina lake ni Askofu Dr. Boaz Sollo.

Wednesday, March 14, 2012

MATENDO MAKUU YA YESU YAONEKANA MBEYA GOSPEL CRUSADE
Umati mkubwa wa wakazi wa mbeya na vitongoji vyake waliohudhuria katika uwanja wa uhasibu mbeya katika mkutano ulioandaliwa na Askofu Boaz Sollo.
Maltitude of people gathered at uhasibu ground during BISHOP BOAZ SOLLO GOSPEL CRUSADE. many were set free from evil spirit.
Askofu Boaz sollo on te picture using the name of Jesus to heal one of the women who was suffering from Demonic spirit.
Askofu Boaz sollo akiwaombea wenye shida mbalimbali kwa jina la Yesu waliohudhuria katika mkutano mkuubwa uliofanyika mbeya tarehe 9 hadi 11 mwezi wa 3,2012
Askofu boaz Sollo akihudumu katika mkutano mkubwa aliouandaa uliofanyika viwanja vya uhasibu mbeya akiwaongoza waliohudhuria kuunyoosha nadhiri zao kabla ya kuziombea ili kupata mafanikio katika maisha.

Mbali na miujiaza mingi kutendeka moja ya muujiza ulioshangaza maelfu ya watu waliohudhuria katika mkutano wa injili wa huduma ya overcpmers power center na kanisa la Endtime Harvest Church inayoongozwa na Askofu Dr Boaz Sollo ni neno la mamlaka alilotoa kuamuru mvua isinyeshe hadi mkutano huo ulipomalizika.

Mkutano huo uliofanyika hivi karibuni katika viwanja vya uhasibu jijini mbeya na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jiji hilo na mikoa ya pembezoni.

Pamoja ni kwamba ni majira ya masika, kwa siku tatu za mkutano huo uliovuta watu wengi kwa Yesu Kristo na kuokoka baada ya kuponywa magonjwa sugu, mvua ilisimama nyakati za jion na kunyesha usiku na asubuhi jambo ambalo askofu Boaz alisema lilidhihirisha jinsi Mungu anavyojibu maombi.